IJUE HISTORIA YA SANAMU YA ASKARI PALE POSTA
"Siku moja majira ya jioni, mishale ya saa kumi unusu hivi maeneo ya Upanga, mmoja wa magiwji wa siasa na mpigania Uhuru wa Tanganyika katika ada yangu ya kumtembelea alinijuza mengi lakini jingine ni pamoja na sanamu la Askari au mnara wa Askari pale Posta.
Historia ya mnara ule inaanza toka mwanzoni mwa miaka ya 1889, kisha kabla na baada ya vita vya kwanza vya dunia mpaka vita vya pili vya pili vya dunia.
Kwa ufupi,Sanamu la mwanzo kukaa pale ni sanamu la Herman Von Wissman,Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir ibn Salim Al Harthi wa Pangani Tanga.
Baada ya kumteka na kumnyonga Abushiri, Von Wissman alirejea ujerumani na kisha baadaye kuteuliwa kuwa Gavana wa nchi zilizo chini ya Ujerumani za Afrika Mashariki.
Aliutwaa mji wa Dar es salamna pwani nzima. Japo alikaa muda mchache Dar es salam.
Gavana huyu alifanya utafiti wa kugundua ni wapi kitovu cha mji wa Dar es salam. Yaani katikati mwa mji kwa vipimo, ndipo akagundua eneo lile pale Posta na kisha akasema pajengwe bustani na sanamu lake likasimikwa.
"Inadaiwa pale ndipo katikati mwa Dar es salam."
Inaaminika ndiye aliyetoa wazo la kujenga ramani ya makambi ya wapiganaji ama wanajeshi wa Jeshi la Ujerumani eneo ambalo lilikuwa likiitwa Carrier Forces(Waswahili wakaita Keriakoo/kariakoo).
Ndo maana utaona mitaa ya Kariakoo imenyooka na kujengeka vizuri. Yalikuwa ni makambi ya wanajeshi.
Basi baada ya vita vya kwanza vya Dunia na Waingereza kushinda na kuchukua koloni la Tanganyika, mwaka 1916 ndipo sanamu la bwana Von Wissman liliondolewa na likawekwa sanamu la sura ya Askari mweusi mwaka 1927 kama ishara ya kuthamini waliopigana kwenye vita hivyo.
Historia ya mnara au sanamu la Askari pale posta nilipewa na Mzee Abbas Abdulwahid Sykes nyumbani kwake Upanga miaka kadhaa nyuma.
Vijana wa aina Goodluck Mlinga mbunge wa ccm huko Ulanga Morogogoro aliyepele hoja Bungeni kwamba serikali ivunje sanamu hii na kujenga sanamu ya mwanamziki Diamond, wanatakiwa kusaidiwa ama kuepushwa na mzigo mzito wa kuwakilisha wananchi mbele ya vyombo vya maamuzi, Niwasihi tuwe na utaratibu kupenda kuwatembelea wazee wenye hazina ya maarifa na historia kuchota elimu hiyo kwao,kwani mengine hatuwezi kuyapata kwenye vitabu wala Google.
0 Comments