![]() |
MAFUNZO YA UJASILIA MALI KWA VITENDO |
Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Vitendo na Mama Irene
Karibu kwenye mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo yanayoongozwa na Mama Irene. Kupitia mwongozo huu, utajifunza kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazouzwa sana mitaani na mashuleni kama sabuni, vikoi, batiki, vitafunwa, na zaidi.
📘 Pakua Kitabu Kamili cha Mafunzo
🧼 SURA YA KWANZA: Utengenezaji wa Sabuni za Maji
✅ Aina za Sabuni
- Sabuni za Kunawia Mikono
- Sabuni za Usafi wa Chooni
- Sabuni za Kufulia
- Shampoo
🧪 Malighafi za Kutengeneza Sabuni ya Kunawia Mikono
- Sulphonic Acid – Inafanana na asali
- Siless – Kuimarisha povu
- Sodaash – Inang'arisha na kuongeza povu
- Formalin – Hifadhi sabuni na kuua bacteria
- Griseline – Inarainisha ngozi
- Perfume – Harufu nzuri
- Rangi – Kuvutia wateja
- Maji – Kibebeo kikuu
- Chumvi – Kuongeza uzito
🛠Hatua za Kutengeneza Sabuni ya Mikono
- Weka lita 10 za maji safi kwenye ndoo
- Ongeza vijiko 3 vya chakula vya sulphonic acid, koroga kwa dakika 5–15
- Weka ½ lita ya Siless, endelea kukoroga
- Ongeza kijiko 1 cha chakula cha Formalin, koroga
- Weka vijiko 3 vya Griseline, koroga
- Ongeza ½ kijiko cha chai cha Rangi (kijani/bluu), koroga
- Weka vijiko 2 vya chai vya Sodaash, koroga
- Ongeza Chumvi ¾ na endelea kukoroga polepole
- Weka vijiko 2 vya Perfume, koroga mpaka sabuni iwe tayari
NB: Acha sabuni ipoe kwa masaa 2, kisha fungasha kwenye chupa/vifungashio. Funika sabuni ili harufu ya perfume isipotee.
📌 SOMA ZAIDI:
Jifunze Utengenezaji wa Sabuni za Miche
🚿 Sabuni za Chooni
Malighafi
- Maji lita 10
- Sulphonic acid ½
- Siless vijiko 5 vya chakula
- Formalin vijiko 5
- Chumvi ¼ kilo
- Sodaash vijiko 4
- Rangi kijiko 1 cha chakula
- Perfume vijiko 2
Hatua za Kutengeneza
- Weka maji lita 10 kwenye ndoo safi
- Ongeza sulphonic acid ½, koroga
- Weka Siless, Formalin, Rangi, Chumvi na Sodaash kwa utaratibu
- Koroga kwa dakika 20–30 bila kuacha mabonge
- Ongeza Perfume mwisho kabisa
NB: Funika na acha ipoe kwa masaa 2 kabla ya kufungasha.
💇 Shampoo
Malighafi
- Sulphonic Acid – Ongeza povu
- Sodaash – Kata acid
- Maji
- Siless – Povutisha na kung’arisha
- Formalin – Dhibiti bacteria
- Griseline – Ngozi laini
- Perfume – Harufu nzuri
- Chumvi – Uzito
- Mayai – Kiini (optional)
Hatua za Kutengeneza Shampoo
- Andaa lita 10 za maji
- Weka sulphonic acid vijiko 4 vya chakula
- Weka Siless ½ kg, koroga dakika 15
- Ongeza Sodaash, Griseline, Formalin, Rangi
- Koroga kwa utaratibu hadi rangi isambae vizuri
- Changanya kiini cha mayai 2 pembeni, kisha changanya na sabuni
- Ongeza Perfume mwisho
NB: Acha ipoe kwa masaa 2 kabla ya kufunga kwa ajili ya kuuza.
20 Comments
Natamani sana kujua namna ya kutengeneza
ReplyDeletekaribu sana
DeleteNawezaje kupata malighafi baada ya mafunzo haya?
ReplyDeletemalighafi zinapatikana kwa hilo ondoa shaka kabisa, wewe uko wapi?
DeleteMwalim ahsante Kwa maarifa hayo nmeongeza kitu kipya kingine Mungu azid kukubark Kwa kutufkia wote Ili tujikwamue kiuchum n kuondokana n umaskn
DeleteAhsante Kwa mafunzo mazur,, naweza kupata malighafi nipo ushetu Kahama
ReplyDeleteMalighafi yanapatikana SIDO kote nchini popote pale ulipo nenda SIDO
Deletenahitaji malighafi ya kutengeneza sabuni hizo. napataje
ReplyDeleteZinapatikana SIDO nchi nzima
DeleteNatamani kujua kutengeneza
ReplyDeleteEndelea kujifunza muda utafika utajua, bidii yako ndio mafanikio yako!
DeleteAsante kwa maelezo mazuri
ReplyDeleteAhsante! Endelea kufuatilia post zingine zinazofuata nitaweka hapa masomo mengine ambayo hujafundishwa popote!
DeleteHellow admin naitaj kujua jinsi ya kutengeneza sabuni ya choon na kufulia ya maji please
DeleteOk
DeleteNzuri san hii
ReplyDeleteKaribu sana nakitabu kipo kama ukihitaji bonyeza link hii https://realjumanne.gumroad.com/l/imwij
DeleteAsante mwalimu kwa ujuzi huu umenifundisha kitu kikubwa sana
ReplyDeleteNaomba namb zako admin nmeshatengeneza sabun ya mche mara mbili lakn haijaganda
ReplyDeleteNaomba namb zako admin nmejarb kutengenez sabun ya mche mara mbili zaid lakn haijaganda
ReplyDelete