1.WAZAZI
Wazazi wengi hawafuatilii kwa ukaribu maendeleo ya watoto wao kitaaluma, hii inatokana na sababu kuwa wazazi wengi wa watoto wa shule za kata si wasomi, upeo wao kuhusu elimu ni mdogo hivyo huona kama ufuatiliaji ni jukumu la walimu shuleni pekee. Hapo ndipo watoto wanapopotea kwa kukosa mwongozo wa ufuatiliaji wa wazazi.
2. UTANDAWAZI
Hakika kama kuna janga kuu katika kuharibu watoto miaka hii basi hili ni namba 1, mitandao ya kijamii na tabia za utandawazi, mitindo, mavazi, movies na nyimbo za muziki zimekua zikifikisha fani zaidi kuliko maudhui, kila mahali kinachohubiriwa ni mapenzi na starehe, watoto nao wanaingia tamaa wanaona cha kufia nini, wanaanza tabia za ajabu ajabu na kupotea kimasomo, hii ndio maana imekua ni jambo la kawaida miaka hii kuwakuta watoto wa shule za kata wamenyoa viduku, wanakunywa viroba, wanavuta bangi, wanatukana,wanabishana na kupigana na walimu /wazazi n. k
3. UMASKINI KATIKA FAMILIA
Hii ni mojawapo ya sababu inayowagusa zaidi wanafunzi wa vijijini na baadhi ya miji, kutokana na umaskini katika familia vijana au watoto wengi wamejikuta wakilazimika kujiingiza katika majukumu mbali mbali ya kutafuta ela wakati huo huo wanasoma, hii inawafanya kushindwa kuwa busy kimasomo, vibarua na kazi ngumu wanazofanya weekend na kila siku baada ya kutoka shule huwachosha kimwili na kiakili pia kisaikolojia wanakosa morali ya kusoma sana kutokana na kukata tamaa wakitazama mbele. Hujiuliza kama chakula tu ni shida je! Ada mbeleni itawezekanaje
4. UMBALI MREFU
Maeneo mengi hakika bado kuna changamoto kubwa ya kimiundombinu, watoto wanatembea umbali mrefu mno kilometa 6 hadi 10 kwenda na kutoka shule, hatimaye huambulia uchovu mkali na kuathirika kimasomo. Wapo wanafunzi wa mijini ambao unakuta anapanda gari 2 hadi 3 ili kufika shule, stendi kwenyewe gari za kugombania na ndani ya hizo gari sometimes makondakta wanawasumbua. Hakika umbali mrefu bado ni tatizo kubwa.
5. UHABA WA WALIMU
Hili ni janga ambalo serikali yapaswa kulitatua kwa vitendo hususani kwa upande wa walimu wa sayansi, shule nyingi za kata zina upungufu mkubwa wa walimu hususani wa sayansi na watalaamu wa maabara. Jiulize mwanafunzi mwaka mzima kafundishwa chemia na bilogia vipindi vitatu tu tena na mwalimu wa tempo je! Kuna kufaulu hapo?
6. JAMII
Jamii inayomzunguka mwanafunzi au mtoto wa shule hususani wa kike ina nafasi kubwa sana ya kumtengeneza au kumharibu, inasikitisha unakuta dereva bodaboda, dereva bajaji au kinyozi wa saloon ana uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi je! unafikiri atasoma hapo? Shule nyingi za kata ni za kutwa(day) hivyo kitendo cha wanafunzi kutoka shuleni na kuingia mtaani huwakutanisha na vishawishi lukuki vinavyowaharibu kimasomo.
7. UHABA WA VIFAA
Shule nyingi za kata hazina vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia, maabara hazijitoshelezi hali ya vitabu nayo ndio hoi bin taabani watoto wanajisomea vitini vya tuition vilivyojaa upotoshaji na notes zisizofuata syllabus hakika kwa mjini hususani mkoa wa Dar es Salaam hili limejidhihirisha kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ambapo pamoja na kuepo tuition centers kibao ila shule 10 za mwisho kitaifa 6 kati yao zatoka Dar.
8. WATOTO WENYWEWE
Wengi wao wamekua wakisoma bila malengo yaani wao kwenda shule kila siku ni kama utamaduni ila hawana mikakati binafsi ya kujisomea kwa bidii ili kufikia malengo yao. Hii ndio maana imekua ni jambo la kawaida kuwakuta wakipoteza mda wao mwingi wakijiingiza katika mahusiano ya kimapenzi, makundi ya vibaka hadi panya road, ngoma za vigodoro, singeli, kuendesha bodaboda, mabanda ya video na michezo ya kubeti.
Kwa leo naomba niishie hapo ila ninaamini ujumbe wangu umewafikia walengwa yaani,
A. Wazazi
B. Jamii
C. Watoto/Wanafunzi
D. Serikali
E. Wadau wote wa Elimu Tanzania
Kama unakubaliana nami kwa hoja nilizowasilisha hapo juu tafadhali comment CHOCHOTE kisha SHARE post hii mpaka imfikie kila Mtanzania atambue wajibu wake katika kufanikisha elimu bora kwa watoto wetu nchini.
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
0 Comments