NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Laana huathiri mafanikio: Ukifanya mambo haya, utapata laana itakayokusababishia mikosi katika maisha yako


Ulishawahi kujiuliza kwanini unaandamwa na mikosi katika maisha yako?

Ulishawahi kujiuliza kwanini unaandamwa na roho ya kukataliwa?

Ulishawahi kujiuliza kwanini unaandamwa na roho ya madeni?

Ulishawahi kujiuliza kwanini ukipata pesa hazikai (ndio mataizo yanajitokeza)?

Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha kutokea kwa hayo. Mfano, pingu za kiutamaduni (ushirikina), laana, masuala ya nyota, kasoro za kibinadamu na kadhalika.

Makala hii, inajikita zaidi katika kuyaorodhesha na kuyachambua mambo mbalimbali ambayo mtu akiyafanya, atapata laana itakayomsababishia mikosi katika maisha yake na mambo mengine niliyoyataja hapo juu.

Kabla ya kuchambua mambo hayo, nifafanue kwa ufupi maana ya neno "laana".

Laana ni nuio au kauli fulani anazozitamka mtu baada ya kukosewa kama adhabu kwa mkosaji. Hiyo ndiyo laana isababishwayo na mwanadamu.

Lakini pia kuna mambo ambayo ukiyafanya, utapata laana ambayo itakusababishia mikosi katika maisha yako.

Epuka sana mambo yafuatayo yatakusababishia laana itakayochochea mikosi katika maisha yako na kuathiri mafanikio na amani yako ya moyo.

  • Ukimdhulumu mtu

Jasho la mtu huzaa mikosi. Machozi na manung'uniko anayoyatoa mtu aliyeumizwa kwa kudhulumiwa, hugeuka laana itakayokuandama katika maisha yako yote na kujikuta kila unachofanya hufanikiwi. Jasho la mtu halijawahi kumuacha mtu salama. Kudhulumu mtu ni jambo ambalo husababisha mikosi katika maisha.

Dhuluma hii inahusisha kumuibia mtu, kumtapeli mtu, kutokulipa jasho la mtu na kadhalika.

Mfano, kuna msichana alikuwa ameolewa na kaka fulani, maisha yao yalikuwa ya 'kuungaunga' sana. Siku moja huyo kaka akaiba hela zote za mke wake, hela ambazo alikuwa anazitunza kwenye kibubu baada ya kazi ngumu za kiwandani na kuamua kutokomea kusikojulikana.

Baada ya miaka miwili bila mawasiliano wala kupiga simu, siku moja akapiga simu kwa mke wake akisema kuwa

"mke wangu naomba unisamehe kwani tangu nichukue hizo fedha, kila ninachofanya hakifanikiwi, kila nifanyalo mikosi inaniandama".

Epuka sana kumdhulumu mtu, utapata laana itakayokusababishia mikosi katika maisha yako.


Ukiua au kutoa kafara.

Damu ya mtu ni laana, damu ya mtu ni mikosi, damu ya mtu ni nuksi.

Ukisikia kuwa kuna vitu havina miguu lakini vinatembea, basi ni damu ya mtu.

Ukisikia kuwa kuna vitu havina midomo lakini vinaongea, basi ni damu ya mtu. Damu ya mtu itatembea na wewe kila kona. Damu ya mtu ina nguvu. Ndiyo maana kuna watu wakifanya mauaji wanakosa nguvu za kukimbia na kuamua kukaa ili wakamatwe. Hiyo ni nguvu ya damu. Damu nzito kuliko maji. Kuua ninakokuzungumzia hapa ni pamoja na kuua mtu, kutoa kafara, kutoa mimba, kutupa watoto na kadhalika.

Hayo yote ni mauaji na madhara yake huhusisha mtu kupata mikosi, kutofanikiwa, kutopata mtoto tena, uchizi, matatizo ya kisaikolojia, ndoto mbaya, kufirisika na madhara kadha wa kadha.

Kuna watu wameua, toka waue akili zao hazijakaa sawa, nusu chizi nusu mtu. Laana ya kuua hiyo.

Epuka sana laana ya kuua kwani itaathiri mafanikio na amani yako ya moyo. Hayo yote tisa, kumi utajibu nini kwa Mungu?

Ukimkana au kumtukana mzazi.

Hakuna laana kubwa hapa Duniani kama kumkana au kumtukana mzazi. Vitabu vya Mungu vinaeleza, 

"waheshimu baba na mama upate kheri na miaka mingi Duniani".

Huoni kuwa ukiwakana na kuwatukana, utapunguza kheri na miaka mingi?

Kuna watu wameshindwa kufanikiwa maisha yao yote kutokana na laana ya wazazi, kuna watu wamekuwa wakipata tabu na misukosuko katika utafutaji wao kutokana na laana ya wazazi.

Kuna matajiri wamefirisika kutokana na laana ya wazazi.

Kuna wasanii na watu maarufu wameshuka kutokana na laana ya wazazi.

Laana ya mzazi ni maneno machache tu yanayoweza kubadili maisha yako na kukupa tabu na misukosuko milele.

Epuka sana kuwakana na kuwaumiza wazazi ili kuepuka hii laana mbaya.

  • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Ukifanya hii dhambi hadi shetani mwenyewe anakukataa. Ukifanya hii dhambi ardhi inakulaani. Pamoja na madhara utakayoyapata, laana hii itakupa pepo la kukataliwa na laana ya uchafu. Usidanganywe na ushamba wa utandawazi na dijitali ukashiriki hii laana. Utapata madhara na utakosa cha kujibu mbele ya Mungu wako.

Utandawazi usiwe chanzo cha wewe kulaaniwa.

  • Kudharau au kuchoma maandiko au vitabu vya Mungu

Mfano, Bibilia, "Quran", na vitabu vingine vya Mungu. Kuchoma vitabu vya Mungu ni laana ambayo inaweza kukupa mikosi, uchizi na kadhalika.

Laana zote hizo huweza kuathiri mafanikio yako kwa njia moja au nyingine.

Epuka sana hizo laana.

SULUHISHO: UFANYEJE ENDAPO TAYARI UMESHIRIKI HAYA?

Mungu wetu ni mwingi wa rehema na huruma, omba msamaha wa kumaanisha na fanya toba ya kutoka moyoni, atakusamehe.

Post a Comment

0 Comments