Barabarani, unakutana na mwanamke mchuuzi masikini mwenye mtoto mgongoni, unashusha kioo cha gari lako na kumuuliza kwa sauti ya kijeshi:
Muuzaji masikini anakubaliana na hali na kukujibu, "Chukua tu kwa bei unayotaka, sijauza chochote tangu asubuhi, walau sasa nipate cha kununulia watoto chakula cha usiku."
Amepata hasara, lakini zaidi anaenda kukununulia pia mfuko wa kuweka bidhaa hizi ulizo nunua. Unamwagiza afanye haraka vinginevyo utabadili mawazo.
Anaomba msamaha, na kwa tabasamu anakukabidhi bidhaa zako, anakubariki pia kwa kumuungisha.
Unamrushia hela na kuchomoka kwa kasi na kumwachia wingu la vumbi na moshi linalomfunika yeye na mtoto. Anakohoa wakati anaweka vizuri fedha kidogo alizopata.
Umaskini haujamwachia uchaguzi.
Umefika sasa kwenye hoteli ya nyota tano, ambapo utakutana na rafiki zako. Unawaambia waagize chakula na vinywaji kadiri wanavyotaka. Wanaagiza vyakula vya gharama kubwa, na mabaki ya chakula ni mengi kuliko chakula walichokula.
Gharama nzima inakua shilingi laki tano. Unalipa bila kuomba upunguziwe, unampa mhudumu tip ya shiligi elfu kumi shukrani kwa chakula alichowahudumia ambacho hamkula hata nusu yake.
Tukio hili linaweza kuonekana la kawaida kabisa kwako, lakini sio la kibinadamu.
Point ni kwamba:-
Kwanini kila mara tunaonyesha tuna nguvu ya kubishania bei wakati tunaponunua kutoka kwa maskini?
Kwanini tunakua wakorofi tunaponunua kwa maskini?
Kwanini tunakua wachoyo tunaponunua kwa wahitaji?
Kwanini tunaonyesha ukarimu kwa wale ambao walahawahitaji ukarimu wetu?
Kwanini tunaonyesha upole na utu tunaponunua kwa watu matajiri ambao wanaona hela yetu kama chenchi ndogo tu?
Kwanini tunaelekeza fedha zetu kwenye bahari ya fedha?
Tafadhali nunua vitu rahisi kwa watu mskini kwa bei ya haki
Wakati mwingine, makusudi lipa na ziada unaponunua kutoka kwao.. Kua na UTU wakati mwingine BARAKA zinatoka kwa watu Masikini. MUNGU NIWETU SOTE ...
0 Comments