Sehemu ya 3: Batiki, Vikoi, Shanga, Hereni na Bangili
Katika sehemu hii ya tatu, tutajifunza kuhusu kazi za mikono zinazoweza kuleta kipato kupitia sanaa kama batiki, kushona vikoi, na utengenezaji wa shanga na mapambo ya kuvaa.
🟣 AINA ZA BATIKI
- Kufinyanga
- Kufunga
- Kukunja
- Kutumia Box au Tofali
🧪 Jinsi ya Kutengeneza Batiki ya Msingi
- Andaa kitambaa (mita 3)
- Changanya maji ya moto, soda ash, rangi, black fixer (gm 30 kwa kila mita 3)
- Loweka kitambaa kwa dakika 15
- Ondoa, kianike juani kisha kipige pasi
🟡 Batiki kwa kutumia Bleach
- Kitambaa cha plain wax mita 6
- Maji kikombe ½
- Bleach vifuniko 3
Changanya bleach na maji, nyunyizia sehemu ya kitambaa au funga mafundo. Acha dakika 10 kisha fua kwa maji baridi na anika kivulini.
🔹 BATIKI ZA PRINTI (wax + vibao)
Tumia mishumaa na vibao vya kuchapa maua. Mchoro unapogongwa juu ya kitambaa chenye wax, hutoa batiki ya kuvutia sana.
🧵 UTENGENEZAJI WA VIKOI VYENYE SHANGA
Malighafi:
- Kikoi
- Shanga za rangi mbalimbali
- Uzi, sindano spesheli
- Kiberiti cha gesi
- Vitambaa vya kuchorea picha
Hatua:
- Andaa kikoi, fumua pande mbili
- Sokota pande kwa urembo
- Tunga uzi kwenye sindano
- Choma shanga juu juu (usiache uzi kuonekana ndani)
- Bandika picha au michoro kwa kutumia chaki
- Tumia kiberiti kuchoma nyuzi zilizotoka
🔵 SHANGA, HERENI NA BANGILI
Malighafi:
- Shanga mbalimbali
- Sindano nyembamba
- Uzi wa shanga au waya wa kutunga
- Mkasi, nozo (clip)
Maelekezo:
- Andaa mpangilio wa rangi ya shanga
- Tunga shanga kwa mtindo wa kuvutia
- Tengeneza bangili au hereni kwa urefu na uzuri unaotaka
- Funga mwisho wa uzi kwa nozo au kifunga spesheli
📌 VIASHIRIA VYA UBORA
- Rangi zinazovutia na kuvumilia kuoshwa
- Mpangilio mzuri wa shanga na picha
- Vikoi vilivyochorwa vizuri na shanga zilizoimarika
Mwisho wa Sehemu ya 3. Tazama Sehemu nyingine hapa chini:
- 🔹 Sehemu ya 2: Sabuni za Miche (Gwanji)
- 🔹 Sehemu ya 4: Vitafunwa (Maandazi, Skonzi, Karanga, Tambi) – Inakuja hivi karibuni!
Hakimiliki ©2025 – Jumanne255. Ruhusa ya kushirikisha ipo, lakini tafadhali usibadilishe chochote bila ruhusa ya mwandishi.
0 Comments