Sehemu ya 2: Utengenezaji wa Sabuni za Miche (Gwanji)
Katika sehemu hii, utajifunza kutengeneza sabuni imara ya miche (magadi/gwanji) kwa hatua sahihi. Sabuni hizi hutumika kwa kufulia au kuogea, zikiwa na rangi nzuri, povu jingi na bila kuwasha ngozi.
🔹 Sifa za Sabuni Bora ya Gwanji
- Iwe na harufu nzuri (kama umeweka perfume)
- Toa povu jingi na la muda mrefu
- Iwe ngumu, imara na isiyovunjika kirahisi
- Iwe na rangi nzuri (bluu/kijani)
- Isiwe na mwasho wa ngozi
- Iwe na shape nzuri na mvuto wa mteja
🔸 Malighafi
- Mafuta ya mawese, alizeti, mise au mbosa – lita 20
- Costic soda – kilo 4
- Maji safi – lita 10
- Sodium silicate – kupunguza mwasho
- Hydrogen peroxide – kuipa sabuni weupe
- Hydrometer – kupima joto la maji + costic (280–300°C)
- Rangi ya sabuni – bluu, mafuta
- Perfume – kwa harufu nzuri
🔸 Vifaa Muhimu
- Box la mbao lenye nailoni ndani
- Beseni au ndoo kubwa mbili
- Mwiko mrefu wa mti au plastiki
- Kisu na meza ya kukatia sabuni
- Gloves, mask, apron (usalama wa mwili)
⚠️ Tahadhari: Usalama Kwanza
- Va’a gloves, mask na miwani wakati wa kuchanganya costic soda
- Usikoroge costic soda sehemu yenye watu au watoto
- Usishike kwa mikono mitupu
- Endapo italipuka au kukuchoma, tumia maji mengi kusafisha
🛠️ Jinsi ya Kuchanganya Costic Soda
- Pima maji lita 10 kwenye beseni kubwa
- Ongeza costic soda kilo 4 polepole huku ukikoroga kwa mwiko
- Koroga kwa dakika 40–45 hadi iyeyuke vizuri
- Acha mchanganyiko huu upoe kwa saa 24 mahali salama
🧼 Jinsi ya Kutengeneza Sabuni ya Miche
- Mimina mafuta lita 20 kwenye ndoo kubwa (yatakuwa yameyeyuka)
- Andaa maji yaliyochanganywa na costic soda (yenye joto sahihi)
- Koroga mafuta polepole huku unamimina mchanganyiko wa costic soda
- Koroga kwa dakika 30 hadi iwe uji mzito
- Mimina kwenye box lililotandikwa nailoni au karatasi ya plastiki
- Changanya rangi na mafuta pembeni kisha mimina ndani ya uji wa sabuni
- Tumia kibao refu kupiga mistari ya mawingu juu ya sabuni
- Acha ipoe kwa saa 24, kisha kata kwa umbo unalotaka
🎨 Namna ya Kutengeneza Rangi ya Sabuni
- Chukua mafuta kidogo (robo lita)
- Changanya na vijiko 6 vya rangi ya bluu
- Koroga hadi ilainike, kisha mimina juu ya sabuni
🆘 Huduma ya Kwanza kwa Ajali za Costic Soda
- Osha mara moja kwa maji mengi ya kawaida
- Usitumie kemikali nyingine
- Tafuta msaada wa matibabu kama athari zitaendelea
📌 SOMA SEHEMU NYINGINE:
- 🔹 Sehemu ya 1: Sabuni za Maji, Chooni, na Shampoo
- 🔹 Sehemu ya 3: Batiki, Vikoi, Shanga na Herini – Inakuja hivi karibuni!
Hakimiliki ©2025 – Jumanne255. Ruhusa ya kushirikisha ipo, lakini tafadhali usibadilishe chochote bila ruhusa ya mwandishi.
0 Comments