Sehemu ya 4: Utengenezaji wa Vitafunwa
Katika sehemu hii ya mwisho, tunakuletea njia za kutengeneza vitafunwa maarufu vinavyopendwa sana: maandazi, skonzi, karanga za mayai, na tambi. Unaweza kuvitumia nyumbani au kuvigeuza kuwa biashara yenye kipato cha uhakika.
🍩 Maandazi
Mahitaji:
- Unga wa ngano – 1kg
- Sukari – ¼ kg
- Baking powder – kijiko 1 cha chakula
- Amira – kijiko 1 cha chakula
- Rangi ya chakula – kijiko 1 cha chai
- Mafuta ya kukandia na kupikia
- Chumvi kidogo na vanilla (ukipenda)
Hatua:
- Umua amira pembeni kwenye kikombe hadi iumuke
- Changanya unga, sukari, baking powder, rangi, chumvi na amira
- Kanda hadi unga uwe laini, funika uumuke kwa dakika 20
- Gawanya na kata umbo la maandazi
- Kaanga kwenye mafuta ya moto wa wastani hadi yawe rangi ya kahawia
🍞 Skonzi
Mahitaji:
- Ngano – 1kg
- Amira – kijiko 1 cha chakula
- Mayai – 2
- Maziwa – ¼ kikombe
- Sukari – vijiko 4 vya chai
- Chumvi kidogo
Hatua:
- Umua amira na gonga mayai kwenye bakuli, changanya vizuri
- Changanya vitu vyote, weka maziwa kidogo kidogo ukikanda
- Kata kama chapati
- Paka mafuta kwenye sufuria, weka mabonge, funika uumuke
- Pika moto wa chini na wa juu kwa utaratibu hadi ziive
🥜 Karanga za Mayai
Mahitaji:
- Mayai – 2
- Sukari – ¼ kg
- Unga wa ngano – ¼ kg
- Karanga – 1kg
- Mafuta ya kupikia
Hatua:
- Changanya mayai na sukari hadi iyeyuke, weka chumvi kidogo
- Weka karanga ndani, nyunyiza unga wa ngano kidogo hadi zipate mchanganyiko
- Kaanga kwenye mafuta ya moto wa wastani hadi ziwe za kahawia
🍝 Tambi
Mahitaji:
- Unga wa dengu – 1kg
- Baking powder – kijiko 1 cha chakula
- Pilau masala – kijiko 1 cha chai
- Pilipili mbuzi – moja (ukipenda)
- Chumvi
- Mafuta, jiko, sufuria, mashine ya tambi
Hatua:
- Kanda unga kupata uji mzito
- Weka kwenye mashine ya kutolea tambi
- Pika tambi kwenye mafuta moto kwa kiasi kinachotosha
- Baada ya kuiva, chuja na pakia tayari kwa kuuza
📌 Hitimisho
Asante kwa kufuatilia mfululizo wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo. Thubutu, jaribu, fanya mazoezi hadi ubobezi. Mungu akuzidishie maarifa, kipato na mafanikio!
Hakimiliki ©2025 – Jumanne255. Ruhusa ya kushirikisha ipo, lakini tafadhali usibadilishe chochote bila ruhusa ya mwandishi.
0 Comments