NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Marafiki wa Kweli Huonekana Maji Yanapofika Shingoni

Marafiki wa Kweli Huonekana Maji Yanapofika Shingoni

Mara nyingi tunajikuta tumegubikwa na makundi ya marafiki, tunaita "squad", tunajivunia kuwa sehemu ya vikao vya kila wiki, safari zisizoisha, na starehe zisizo na mwisho. Lakini hebu jiulize swali moja dogo lakini zito: Ni nani atakayebaki na wewe siku ukiwa huna kitu?

Nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba ikiwa unajiona wewe ni mbinafsi lakini unafikiri ni kawaida kwa sababu wengi wapo hivyo, basi unapaswa kujiuliza tena. Kuna maisha baada ya starehe, kuna maisha baada ya kazi, kuna maisha baada ya umaarufu – na siyo maisha yote ni mazuri. Wakati mwingine huanguka. Na hapo ndipo unapoanza kutofautisha ujamaa na urafiki wa kweli.

Kazi Ulionayo Leo, Ni Daraja Tu

Kazi unayofanya sasa haikupi kinga ya changamoto. Inaweza kuwa nzuri, inalipa vizuri, lakini haitabiriki. Unaweza kufukuzwa, ukaumwa, au hali ikabadilika ghafla. Katika hali kama hiyo, wale marafiki wa kweli ndio wanatambulika – sio wale wa vicheko vya kila siku, bali wale wa machozi yasiyo na wingu.

Marafiki wa Bia si Marafiki wa Maisha

Wengi mnajivunia kuwa na squad, lakini huwezi kumtaja hata mtu mmoja ambaye unaweza kumpigia simu ukiwa hospitalini, ukiwa umepoteza kazi, au ukiwa umefilisika.

Marafiki wa kweli hawapimwi kwa wingi wa picha mliopiga pamoja, bali kwa ushuhuda wa nyakati ngumu. Rafiki wa kweli ataumia pamoja na wewe. Atafunga pamoja na wewe hata kama si kwa imani yako – kwa sababu uchungu wa mwenzake umekuwa wake pia.

Chunguza Mduara Wako (Circle)

Jiulize:

  • Ukianguka, nani atakusimamia?
  • Ukiwa huna kitu, nani atakusaidia bila kujisifu?
  • Ukiwa mgonjwa, nani atakutembelea bila kulazimishwa?

Hii ndiyo mizani ya urafiki wa kweli. Tofautisha marafiki wa vibes na marafiki wa value.

Hitimisho

Tunaishi katika dunia ya kuigiza. Watu wanapenda kuonekana wako karibu nawe kwa sababu ya kile unacho – si kwa sababu ya wewe kama wewe. Lakini ukipoteza hicho wanachokitafuta, basi watapotea kabla hata hujawakosa.

Jifunze kupima marafiki si kwa maneno yao, bali kwa matendo yao. Kuwa makini na circle yako. Hakikisha unawazungukwa na watu wanaokuombea mema hata nyuma ya pazia, wanaoweza kutoa sadaka ili usipotee, na wanaojivunia kusema “huyo ni rafiki yangu” hata ukiwa kwenye mavumbi.

Post a Comment

0 Comments