Msajili wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi ameviagiza vyama vyote vya siasa nchini kusitisha mikutano na makomangano hadi hapo mkutano huo wa wadau wa siasa utakaoitishwa na IGP hivi karibuni ufanyike.
“Tunafanya jitihada kuondosha mvutano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa, Msajili kama Mlezi wa Vyama vya Siasa niliwasiliana na IGP na tukakubaliana tuwaite Wadau, katika kikao hicho tutawaita Polisi wakiongozwa na IGP, Viongozi wa Vyama pamoja na Ofisi ya Msajili” Jaji Mutungi
“Lengo la kikao cha pamoja kati ya Polisi, Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama ni kukaa chini kuwa na maongezi kuhusiana na mikutano, makongamano n.k, nisingependa ifike mahala Watu waanze kuogopa, kila Mkutano wa Siasa Mapolisi wamejaa” Jaji Mutungi
“Siasa ya Nchi yetu haijafikia hatua hiyo ya taharuki ambazo hazina mbele wala nyuma, ni suala tu la kuwekana sawa, tunataka kuondoa hicho kitu ambacho Polisi wanaona Wanasiasa wanakosea hapa na Wanasiasa wanaona Polisi wanakosea hapa” Jaji Mutungi
“Niwakumbushe tu licha ya Mkutano unaokuja kati ya Polisi, Vyama na Msajili, bado kuna fursa nyingine ambayo Wanasiasa wanayo ya kukutana na Rais kama alivyoahidi kukutana na Wanasiasa kama kuna changamoto nyingine huo ni muda mwafaka wa kuzitoa” Jaji Mutungi
“Wanasiasa ni wasikivu wala tusiwajengee taswira kwamba ni Watu wasio na uchungu na Nchi, wanao uchungu na Nchi na pia tusivijengee taswira hasi vyombo vya ulinzi kwamba hawana uchungu na Nchi hii” Jaji Mutungi,
“Wanasiasa nawaomba wawe na subira, nisingependa kusikia kesho tena kuna kongamano limeandaliwa mahali, watupe nafasi muda si mrefu ujao tutakuwa na kikao hicho muhimu cha Wadau kitakachowahusisha Polisi, Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili” Jaji Mutungi
0 Comments