PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF ZAMBIA HAIKANDE HICHILEMA |
"Sala yetu tunapojiandaa kwa ajili ya sherehe za uapisho.
Mungu Mtakatifu, Wewe uliye asili ya Uzima na Uhuru, Muumba wa vyote, jina lako litukuzwe duniani na mbinguni, sasa na hata milele.
Kwa hekima yako isiyo na kikomo, umeniweka kuwa kiongozi wa watu Wako leo, ninapojiandaa kuapishwa katika ofisi ya juu kabisa ya nchi yetu, ofisi ya Urais.
Sijiombei chochote ila unyenyekevu, hekima na maarifa ya kuwatumikia watu wako, hekima na maarifa uliyompa Mfalme Suleiman wakati alipoitafuta na kukuomba, katika 2 Mambo ya Nyakati 1:10;
"Nipe hekima na maarifa ya kuwaongoza vizuri, kwani ni nani awezaye kutawala watu wako hawa wakuu?"
Lakini pia ninawaombea maafisa wetu wa serikali, wale wanaotumikia katika nafasi za majukumu makubwa na wale wa majukumu madogo, wale wanaowakilisha mamilioni na wale wanaotumikia mamia, wale ambao maamuzi yao yataathiri vizazi na vizazi hata ambavyo bado havijazaliwa, na wale ambao wanahudumu nna kutumika katika mahitaji ya leo.
Utujalie sisi tuweze kuwatendea matajiri na masikini, vijana na wazee, mjane na yatima, wasomi, na wasio wasomi, wapinzani wetu wa kisiasa na comrades, kwa heshima, haki na upendo.
Na tuhudumu bila ubaguzi au upendeleo wakati wa mafanikio au umaskini, amani au wakati wa tofauti zozote tutakazokutana nazo. Ee Mungu, kila mmoja wetu kama viongozi tuwe watu wa uadilifu, uaminifu na kujitolea; ambao hutumikia kwa huruma ya kweli, hawatafuti faida ya kibinafsi, hadhi au ufahari.
Na tufanye kila juhudi kufanya jamii yetu, majiji yetu, na taifa letu, sio tu kuwa mahali bora pa kuishi, lakini kuwa mahali bora panapojulikana kuwa na sifa ya huruma na haki.
Mpe kila mmoja wetu maarifa, ufahamu, ujasiri na nguvu. Naomba tujue mema na mabaya, wakati wa kubadilika na wakati wa kuwa thabiti.
Baba wa Mbinguni, ihurumie ardhi yetu tukufu na kwa wale ambao tunaongoza katika jamii zetu, miji, na serikali ya kitaifa. Mkumbushe kila mmoja wetu wito wake alioitiwa. Ili kila mmoja aipe thamani ya juu haki, uaminifu, uadilifu na huduma anayoitoa.
Wote wawe na moyo safi na amani na furaha ya kujua wamechagua njia kuu. Ee Mungu, hakuna mtu aliyesema itakuwa rahisi na hakuna mtu aliyesema itakuwa ngumu sana. Lakini na iwe siku ifike wakati tunaweza kusema, "Bwana asifiwe, Hossanna huko juu, tumetoka mbali, tumefika mbali na tunaenda mbali!"
Tunakuomba haya kwa jina la MUNGU Mwenye haki wa wenye haki; aliye safi kuliko wote, Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.
Wananchi wenzangu,
Nawatakia sherehe njema za siku ya uapisho. Leo ninasaini maombi yangu haya kama Rais Mteule, lakini kesho nitaitia saini kama Rais wa Jamhuri ya Zambia. Heshima, sifa na utukufu ni kwa MUNGU, tangu milele hata milele. Amina. Mungu akubariki na aibariki Jamhuri ya Zambia.
Hakainde Hichilema
Rais Mteule.
Jamhuri ya Zambia. "
Imetafsiriwa na
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
0 Comments