NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

SIYO POLISI TU, HATA WEWE NI MSHENZI TU!



Angalizo, kama unahasira za haraka kama mtu asiye na hela usisome! Usisome! Povu ruksa!

We sindiyo tangu upewe hiyo ofisi unataka kumlala kila msichana anayekuja kuomba kazi hapo?  Yako huyaoni, unaona ya polisi! Shame!Ina maana wasichana warembo hawana haki ya kupata kazi?

We sindiyo umemdhulumu house girl anayekutunzia watoto wako? Siku alipokuomba pesa ukamzushia ati ni mchawi, leo unaona ushenzi wa polisi! Bure kabisa. Akinyonga watoto wako unakimbilia polisi wakusaidie! Chefuu!

We sindoyo umewadhulumu wafanyakazi wako baada ya kukutajirisha? Watu kazi wamefanya, mafao yao umekula halafu unafungua mdomo kuwalaani polisi. Ama kweli mchawi haoni kundule.

We sindiyo unamchuna mume wa watu hadi ameshindwa kutunza familia yake? Umekomaa hadi kakununulia gari la mkopo na wakati mke wake hata bajaji hana. Hivi unatoa wapi jeuri ya kuwashambulia polisi?

We sindo umekula posho za washiriki wa mkutano wa maendeleo? Au unadhani hatujui? Bora ukae kimya tu ukirekebisha tabia zako za kishenzi! Unajimaliza!

We sindiyo unaomba ngono kwa kila anayetia nia kupitia chama chako? Hivi hao unaowaomba ngono hujui kama wana wame zao na boyfriend zao? Unadhani wanakuonaje? Leo polisi kuomba ngono huko Tanga unatamani kufa! Acha zako bana!

We sindiyo uliapa kutotoa 'A' darasani na wakati wewe wakati unasoma ulipewa A, hukufanyiwa mtimanyongo. Halafu somo lenyewe unalofundisha ni mboga tu. General Studies! Je ungekuwa unafundisha hesabu, sindio ungeua wanafunzi? Acha ushamba!

We sindiyo umefelisha kila msichana aliyekunyima? Unadhani hatuna taarifa zako? Huo ni ufala ufala. Vya watu haviliwi kizembe namna hiyo!

Lakini hata nyie polisi mnazingua. Acheni bhana. Hivi hamkui laana ya hayo itakuwa juu yenu na juu ya watoto wenu. Kuna watu wanapitia magumu kumbe walikuwa watoto wa polisi!

We sindiyo ukikopa hulipi? Unadaiwa kila baa, unadaiwa kila bucha, unadaiwa na kila dalali, unadaiwa na kila kikoba, unadaiwa Songesha, Unadaiwa Mpesa na nipige tafu na hutaki kulipa. Huo siyo uonevu? We vipi? Acha kutuzingua!

We sindiyoo umesababisha nyumba ya familia kupigwa mnada baada ya kukopa vikoba na kushindwa kulipa? Hizo hela za vikoba siulikula peke yako? Halafu leo unasema una machungu na polisi. Hivi unajia nakushangaa?

We sindiyo unatesa madereva wako? Mtu anakuendesha libasi lako masaa 15 bila kupumzika halafu unamcheleweshea posho yake kisa alipakiza abiria njiani bila kukupa taarifa. Posho zenyewe unazompa huyo dereva hazitoshi chakula cha kuku halafu unawasema polisi. Yaani we ndio usiseme kabisa.

Hivi unadhani hatujui kama we ndiyo ulifilisi duka la watu? Sasa  unatofautiana nini na wauaji? Hilo duka ulilofilisi ndio lilikuwa linasomesha watoto wake, linalisha mke wake, linatibisha wazazi wake, wewe umakata mirija. Mpaka hapo unadhani unauhalali wa kumnyoshea kidole polisi?

We sindiyo mwizi wa dawa na mitungi ya oksijeni pale hospitali? Hivi unajua umeua watu wangapi? Nakushauri utumie muda huo kutubu kuliko kuwalaani polisi. Polisi achana nao,watajuana na Mungu wao. Wao siwajanja? We waache tu!

We sindiyo ulichoma shule na baadhi ya wanafunzi wakafia humo? Hivi uliishatubu dhambi hiyo au umekazana kuwalaani polisi? Huna akili ujue??? Unaona mchanga kwenye jicho la polisi na wakati kwako kuna jiwe. Loh!

Sasa ngoja nikuibie siri; kila ushenzi unaoufanya lazima ukurudie kabla hujafa!

Mungu amekuinua ukatumikie watu wewe unawatumia, hawezi kukuacha salama. Ni suala la muda tu we subiri. Ipo siku nawe utatumika!

Umepewa dhamana ya kulinda watu wewe unawawinda, huwezi kubaki salama. Time will tell!

Mungu amekupa pesa zikufae maishani wewe unazitumia kuiba mademu za watu, unazitumia kutesa watu, unazitumia kudhulumu watu; hii lazima ile kwako. Utaniambi tu!

Sikiliza, laana siyo lazima itoke kwa Mungu, laana inaweza kutoka kwenye mdomo wa mtu yoyote kwa sababu Mungu huwatumia watu kulaani na kubariki. Kazi kwako!

Tatizo mna masikio lakini hamtaki kusikia. Uzuri kusikia kwa kenge ni hadi aone damu inatoka masikioni! Siku yakikufika utaosikia. We endelea!

Mungu amekuhurumia akakupa nafasi ukawafundishe wengine, wewe unawafelisha kwa sababu wamekunyima vya sirini. Unafeli sana bro! Acha. Hivi uliishajiuliza ni wangapi wana akili kukuzidi lakini hawajapewa hiyo nafasi uliyonayo?

Unanyanyasa watu kwa kutumia umaarufu wao, huo ni ushamba! Huo umaarufu Mungu amekupa ili uutumie kusaidia ndugu zako wanaoishi kama washikina! Unadhani hatuwajui?

Karne hii bado kuna watu wanatumia ndugu zao kutishia watu, huo ni ushamba! Yaani mkizinguana kidogo tu unampigia mpenzi wake anayefanya kazi ikulu kukushughulikia na unashughulikiwa kweli! Ipo siku na wewe utashughulikiwa na ikulu, subiri tu mdundo wa ngoma ubadilike!

Eti unamla maskini kabisa!!! We endelea. Hakuna chozi la maskini linalopotea bure. Ipo siku utasikia tu.Hasa ile siku machozi ya maskini yatakapogeuka chungu cha kukupikia maana kichwa cha mbuzi husikia kikiwa chunguni! Usicheze na mnyonge. Mnyonge hana cha kupoteza zaidi ya manyanyaso yako!

We simjanja wa kula vya watu kwa kutumia cheo chako? Walahi nakwambia, kalabla hujafukuzwa kazi hapo lazima ushuhudie mkeo akilalwa na washenzi wenzako.

Nasema hivi kabla hujafa lazima ushuhudie binti zako wakilalwa. Hiyo ndiyo kanuni ya Mungu! Ukitenda ushenzi lazima utendewe ushenzi! Ndiyo maana King J alisema usimfanyie mwenzako kili usichopenda kufanyiwa. King J ni Jesus, yaani Yesu!

Nyie waoneeni watu tu! Ipo siku yaja! Acha mie niendelee kujiuzia vitabu! Rusha 5,000 kwa Mpesa 0753665484 nikurushie kitabu kimojaa kati ya hivi;

1. Ukombozi wa Fikra
2. Maisha ni Kutafuta si Kutafutana
3. Wasomi Huru Gerezani
4. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika
5. Viongozi wanaoishi  Baada ya Kufa!

Wako
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa karne ya 21

Post a Comment

0 Comments