NEW

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Blood Pressure Basics

SHINIKIZO LA DAMU (BLOOD PRESSURE)

Shiniikizo la chini la damu (low blood pressure)

Watu wengi wanadhani shinikizo kubwa la damu na jinsi ya kukabiliwa na tatizo hili pindi linapo wakumba lakini pia ni vyeme kufahamu kwamba shinikizo dogo la damu nalo linahatari sawa.

Pindi shinikizo la damu linapokuwa chini ya kiwango halisi cha 120/80 huchukuliwa kama shinikizo dogo la damu katika mwili wa mwanadamu. Tatizo hili hutokana na msukumo mdogo wa oxygen kupitia kwenye damu kwenda katika moyo na ubongo. Matokeoyake mwili hushindwa kufanya kazi kwa ufasaha na kupoteza nguvu.

DALILI ZA SHINIKIZO DOGO LA DAMU

Hakuna dalili za moja kwa moja kwa tatizo la shinikizo la damu katika mwili wa mwanadamu kwani wahanga wengi wa ugonjwa huu wamekuwa hawaonyeshi ishala kama ilovyo kwa magonjwa mengine. Lakini kitaalamu yapo mambo kadhaa ambayo yanaashiria uwezekano wa mtu kuwa na shinikizo dogo la damu kama ifuatavyo:

  • Mabadiliko kwenye mapigo ya moyo
  • Macho kubadilika rangi
  • Kuhisi kiu mda mwingi
  • Ngozi kubadilika rangi
  • Kupoteza fahamu
  • Kushindwa kuvuta hewa vizuri
  • Kuhisi homo
  • Umakini mdogo

VISABABISHI VYA MSUKUMO MDOGO WA DAMU

Tafiti za wataalamu wa masuala ya afya zinafafanua kuwa tatizo la ugonjwa wa shinikizo dogo la damu hutokana na sababu zifuatazo kwa mwanadamu.

Baadhi ya madawa:

Kuna baadhi ya madawa yanayotumiwa na wanadamu huchochea matatizo ya msukumo wa damu mfano diurestics ambazo hutumika kutibu tatizo la shinikizo kubwa la damu,madawa ya kutibu matatizo ya moyo kama beta blockers na angiotensin yanaweza kusababisha tatizo hili.

Matatizo ya moyo: Matatizo ya moyo wakati mwingine nayo husababisha uwepo wa msukumo mdogo wa damu mwilinmi baada ya kushindwa kusukuma damu ipasavyo kuelekea sehemu zingine za mwili.

  • Kupungukiwa damu
  • Baadhi ya maambukizi
  • Matatizo ya mzio

TIBA YA ASILI MSUKUMO MDOGO WA DAMU

Tiba ya tatizo la msukumo mdogo wa damu hutegemeana na chanzochake hususani kama tatizo limekuwa sugu. Msukumo wa damu ambao unatokana na mzio, maambukizi au mshituko huhitaji tiba makini zaidi. Lakini zifuatazo ni baadhi ya vidokezo muhimu vinavyo weza kusaidia katika kutibu tatizo hili:

  • Usimame eneo moja kwa mda mrefu
  • Epuka mazingira kame na yenye joto
  • Kula chakula kiasi lakini kilichokamilika ikiwa bado shinikizo dogo la damu linazidi kukusumbua jaribu kuonana na daktari kwenye kituo cha afya na kumpa histiria ya mabadiliko yako kiafya bila kificho chochote.
  • Kunywa maji mengi kwa siku. Wastani wa glasi sita mpaka nane kwa siku.
  • Fanya mazoez ya kukimbia au kutembea kwa miguu ili kuruhusu mzuko wa damu mwilini kufanya kazi kwa ufasaha Zaidi.
  • Tumia viungo kama binzari, tangawizi, pilipili kuogeza msukumo wa damu mwilini.
  • Tumia chamvi ya kutosha ili kurejesha kiwango  cha electolytes ambacho kimepotea mwilini.
  • Tumia juisi ya limao iliyowekwa sukari kiasi.
  • Shiriki baadhi ya michezo kama YOGA kwani husaidia kufanya mzunguko wa damu uwe katika hali nzuri.

AINA YA VYAKULA UNAVYO PASWA KULA:

Ufuatao ni utaratibu wa vyakula ambavyo vinapaswa kutumiwa na mgonjwa wa shinikizo dogo la damu ili kuweza kupambana na tatizo hilo.

Punguza kula vyakula vya wanga kama viazi, wali na mikate.

Kahawa inatajwa kuongeza msukumo wa damu mwilini lakini ni vema ukapata ushauri wa daktari kabla ya kuitumia kutokana na vyenyewe kuwa kisababishi vya matatizo mengine ya kiafya.

  • Tumia vyakula venye asili ya chumvi ili kuboresha mzunguko wa damu mwailini.
  • Kunywa kiasi kikubwa cha maji kwa siku kuanzia glasi sita mpaka nane.
  • Kula vyakula vyenye protini na vitamin B  complex na vitamin C vikiwemo mayai, maziwa, nyama. n.k

SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (HIGH BLOOD PRESURE)

Watu wengi wanafahamu  madhara ya shinikizo kubwa la damu na jinsi ya kukabilina na tatzo hilo pindi linapokumba lakini pia ni vyema kufahamu kwamba shinikizo kubwa la damu lina hatari kubwa kwa mwanadamu.

Pindi shinikizo la damu linapokuwa juu ya kiwango halisi cha 120/80 huchukuliwa kama shinikizo kubwa la damu katika mwili wa mwanadamu. Tatizo hili hutokana na msukumo wa damu kwenda katika moyo na ubongo. Matokeo yake mwili hushindwa kufanya kazi kwa ufasaha na kuelemewa.

DALILI ZA SHINIKIZO KUBWA LA DAMU

Hakuna dalili za moja kwa moja  kwa tatizo la shinikizo kubwa la damu katika mwili wa mwadamu kwani wahanga wengi wa ugonjwa huu wamekuwa hawaonyeshi ishara za wazi kama ilivyo kwa magonjwa mengine. Lakini kitaalamu yapo mambo kadhaa ambayo yanaashiria uwezekano wa mtu kuwa na tatizo kubwa la shinikizo la damu endapo litakuwa limekomaa na kufikia hatua ya hatari kama ifuatayo.

  • Mabadiliko kwenye mapigo ya moyo na kuwa ya juu kupita kiasi.
  • Kuumwa kichwa.
  • Kichefuchefu
  • kutapika
  • Kizunguzungu
  • Kuona maruweruwe

VISABABISHI VYA MSUKUMO MKUBWA WA DAMU

Shinikizo la juu la damu huwa linasababishwa na vitu vingi lakini sababu zilizokuu zinaweza kuwa mojawapo au zaidi ya hizi zilizo ainishwa hapo juu.

  • Unene uliopita kisi
  • Kutokuwa na mazoezi ya kutosha
  • Msongo wa mawazo na hofu ya mfululizo
  • Magonjwa ya figo
  • Mabadiliko ya mfumo wa homoni
  • Udhibiti mbaya wa matumizi ya sukari
  • Mshituko wa ghafla

MADHARA YA MSUKUMO MKUBWA WA DAMU

Mara nyingi msukumo wa damu hupelekea madhara yafuatayo:-

  • Shumbulio la moyo (heart attck)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Ini kushindwa kufanya kazi (Liver failure)
  • Kiharusi (strocke)
  • Macho kuharibika
  • Mguu au mkono kuuma mfululizo

TIBA YA MSUKUMO MKUBWA WA DAMU

Endapo umeanza kuhisi dalili za kuwa na tatizo hili au umepimwa na ukakutwa na tatizo hili ikiwa katika hatua za mwanzo, ni rahisi kulitibu endapo utafuata maelekezo yaliyo hapo chini

Lakini kabla ya kuanza kufuata maelekezo hayo, vyema kupata ushauri wa daktari wako kwanza juu ya uwezo wa mwili wako kustahimili tiba za mbadala na kama utatakiwa kutumia dawa za hospitali ni vyema kumaliza tiba za hospitali kwanza kabla ya kuanza tiba hii.Lakini njia hizi zina faa hata kwa wale wanaohitaji uwezekano wa wao kulipata tatizo hili kwa siku za usoni hatakama hawana tatizo hilo.

1.      Fanya mazoezi ya nguvu: Njia hii huweza kupunguza kiwango cha mafuta kwenye moyo na mishipa ya damu hivyo huweza kusaidia kuepuka na matatizo ya kupatwa na shinikizo kubwa la damu mwilini.

2.      Epuka matumizi ya chumvi: Ni ukweli usiopingika kwamba chumvi inaongeza madini ya joto mwilini na kuleta ladha kwenye chakula lakini inapaswa kupunguzwa kwani pia inaweza kupelekea madhara ya kupatwa na shinikizo kubwa la damu ikiwa itazidishwa  Inashauriwa kutotumia chumvi mbichi kwenye chakula.

3.      Kunywa pombe kiasi na ikiwezekana acha kabisa: Ulevi ulio kidhiri huleta matatizo mengi kwenye afya ya mwanadamu ikiwemo mapigo ya moyo kwenda mbio na kuchochea ugonjwa wa shinikizo kubwa la damu mwilini hivyo ni vyema kuepukakana na ulevi ulevi ulio kithili.

4.      Fanya kazi za nguvu: Kitendo cha kukaa kwenye ofisi kwa mda wa masaa 41kwa wiki bila kutoka jasho kinaweeza kukuweka kwenye hatari ya  kupatwa na msukumo mkubwa wa damu hivyo ni vyema wakati mwingine kufanya kazi za nguvu ili kujiweka fiti dhidi ya maradhi kama haya.

5.      Jiburudishe na muziki: Wakati mwingine wa mawazo hupelekea shinikizo la damu hivyo ni vyema kuiburudisha akili yako na aina ya muziki unayoipenda ili kuondoa mawazo yanayoisumbua akiri yako. Kwa kufanya hivi unaweza kupunguza shinikizo kubw la damu.

6.      Jenga utaratibu wa kutembea kwa miguu: Kwa kawaida utembeaji kwa miguu husaidia tatizo la shinikizo la damu kwa mwanadamu. Inashauriwa walau kutembea mwendo wa nusu saa kwa siku ili kuufanya moyo wako upate hewa na kutosha na kusukuma damu vizuri. Jaribu kuongeza kiwango cha kutembea kadri siku zinavyozidi kwenda.

7.      Anza kutumia viazi: Matumizi ya viazi, matunda na mboga zenye kiwango kikubwa cha potasiamu zinaweza kusaidia kupunguza tatizo la shinikizo kubwa la damu mwailini. Tumia potasiamu kwa kiwango cha miligramu 2,000 mpaka 4,000 kwa siku. Madini haya unaweza kuyapata kwa kula chakula kama viazi vitamu, nyanya, juisi ya machungwa, ndizi maharage.

8.      Tumia chocolate nyeusi: Tafiti zinaonyesha kuwa chocolate nyeusi husababisha mishipa ya damu kuwa minyumbufu na kusaidia kupunguza kiwango cha msukumo mkubwa wa damu mwilini.

Post a Comment

0 Comments